Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani.

Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani.
kiungo : Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani.

soma pia


Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani.

Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha wa USD 300,000 ameshindwa kufika katika Mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.

Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika lakini amepewa taarifa kuwa Aveva anaumwa.

Mbali ya Aveva mshtakiwa mwingine ni katibu wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'  Swai ameeleza kuwa amepewa taarifa kutoka Magereza kuwa Aveva hakufika mahakamani kwa sababu ana matatizo ya figo.

Aliongeza kudai kuwa bado hawajapatiwa nyaraka walizoziomba kutoka ofisi ya Aveva na pia aliiomba mahakama iwaruhusu wakamuhoji mshtakiwa Kaburu.

Baada ya hayo, Hakimu Nongwa alikubaliana na maombi ya kutaka kumuhoji mshtakiw kaburu na kuwataka wafuate utaratibu. kesi hiyo imeahirishwa hadi January 25,2018.

Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya Machi 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.


Hivyo makala Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani.

yaani makala yote Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/rais-wa-simba-ashindwa-kutokea.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Rais wa Simba ashindwa kutokea Mahakamani."

Post a Comment