title : NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU.
kiungo : NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU.
NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU.
Na Mwandishi wetu
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amezitaka Halmashauri na Manispaa zote nchini kuzipa kazi ya kukusanya ushuru wa samaki na mazao yatokanayo na samaki BMUs ili ziweze kujiendesha na kusimamia ipasavyo Rasilimali za Uvuvi.
Ulega ameyasema hayo katika Mkutano wa kuzungumza na Jamii ya wavuvi Kilwa - Kivinje.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa ameahidi kuzipa kazi hiyo ifikapo Mwezi Machi, 2018 baada ya kukamilisha zoezi la Upitishaji wa Kanuni ndogondogo kwa kila BMUs ambapo kwa wilaya ya Kilwa zipo sita (6).
Aidha, Mhe. Ulega amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa kuhakikisha kuwa Mtambo wa Kuzalisha barafu katika mwalo wa Kilwa - Masoko unafanya kazi ndani ya siku 14.
Akijibu maswali na hoja za wananchi huku akishangiliwa, Mhe. Ulega, amewaahidi wananchi katika Wilaya hiyo kurudi mwezi Machi kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa.
Katika kuhitimisha ziara yake Mhe. Ulega ameshiriki zoezi la Upigaji Chapa Mifugo katika kijiji cha Mpara, eneo la magereza ambapo kwa siku ya leo tu tarehe 10/01/2018 Jumla ya Ng'ombe 198 wamepigwa Chapa. Jumla ya ng'ombe 40,000 wanatarajiwa kupigwa Chapa katika wilaya ya Kilwa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi katika soko kuu la samaki la mkoa wa Lindi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na watendaji mbalimbali, wavuvi ambapo amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa kuhakikisha kuwa Mtambo wa Kuzalisha barafu katika mwalo wa Kilwa - Masoko unafanya kazi ndani ya siku 14. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwaelekeza namna bora ya kupiga chapa mifungo ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishiriki zowezi la upigaji cha mifungo kijiji cha Mpara mkoa wa Lindi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Zabron Bugingo(katikati) akishiriki zowezi la upiji chapa mifungo, kushoto ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishuhudia zowezi hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kilwa,Zabron Bugingo (wakwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega kuhusu mkakati wa Halmashauri wa kuongeza uzalishaji wa Mikorosho katika kituo cha Mpara.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU.
yaani makala yote NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/naibu-waziri-aagiza-halmashauri.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI, MANISPAA KUZIPA BMUs KAZI YA KUSIMAMIA UTOZAJI USHURU."
Post a Comment