Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote.......

Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote....... - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote......., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote.......
kiungo : Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote.......

soma pia


Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote.......


VYUMA vimekaza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya utajiri wa staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kudaiwa kwisha baada ya magari ya thamani aliyokuwa akiyamiliki kupukutika, Risasi Jumamosi linakupa mkanda kamili.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu ambaye ni mmoja wa watu wa karibu wa Nay, kwa sasa mwanamuziki huyo ana hali ngumu kimaisha kwani ule utajiri aliokuwa nao awali, kwa sasa haupo tena, umepukutika.
“Kiukweli mambo ni magumu sana kwa Nay kwa sababu magari yote aliyokuwa nayo ameuza na sasa amebaki na moja tu, ndiyo maana hata huoni akiwa na mbwembwe kama zamani, hapana chezea hali ngumu ya sasa wewe,” kilisema chanzo hicho.

VIPI KUHUSU STUDIO YAKE?
Mnyetishaji huyo alizidi kutiririka kuwa, hata kwenye studio yake iliyopo Sinza-Kijuweni, Dar, kwa sasa wapo wakurugenzi wawili na kila mmoja ana timu yake ambapo mmojawapo ni Nay na mwingine alitajwa kwa jina moja la Isihaka.
“Studio kwake kwenyewe siku hizi hata hapaeleweki maana kuna uongozi wa watu wawili na kila mmoja ana watu wake. Kuna kipindi wanashindwa kuelewana katika mambo f’lani ya kiutendaji na vikao vimekuwa vikiwekwa kila kukicha,” alisema mtoa habari wetu.

NAY ANASEMAJE?
Ili kuujua ukweli, gazeti hili lilimtafuta Nay ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Risasi Jumamosi: Kuna habari kwamba umefulia na ule utajiri wako wote umepukutika, hili likoje?
Nay: Ni kweli nimefulia.
Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu ishu ya kuuza magari na kubaki na moja tu?
Nay: Hata hilo gari moja sina kabisa, yote niliyauza tangu mwaka jana!
Risasi Jumamosi: Nini kisa cha kuyauza?
Nay: Nimefulia jamani.
Risasi Jumamosi: Kutokana na hali hiyo ngumu, inaelezwa kwamba hata kwenye studio yako mko wakurugenzi wawili, wewe na Isihaka ili kumudu gharama za uendeshaji, hili likoje?
Nay: Duh! Siyo kweli, aliyewaambia amewadanganya.
Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu hii ishu kwamba magari yanayoonekana kwenye video za nyimbo zako siyo yako ni ya huyo Isihaka?
Nay: Duh! Hiyo kali sana, sasa kwenye video kuna msanii anayetumia magari yake binafsi? Huwa tunakodisha, huyo mmbeya wenu amewadanganya.
Baadhi ya magari ambayo Nay aliwahi kuripotiwa kuyamiliki ambapo kwa sasa hana ni pamoja na Range Rover Sport, Toyota Prado, Nissan Murano, Toyota Mark X, Toyota Brevis, Toyota Noah na mengineyo. Pia alikuwa na daladala kadhaa, Bajaj na bodaboda. 


Hivyo makala Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote.......

yaani makala yote Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote....... Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote....... mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/kweli-vyuma-vimekazanay-wa-mitego-akiri.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Kweli Vyuma Vimekaza...Nay wa Mitego Akiri Kufulia na Kuuza Magari yake yote......."

Post a Comment