CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE

CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE
kiungo : CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE

soma pia


CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel ambayo inajenga jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi kuhusu maendeleo ya mradi huo alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.

Na Hamza Temba - WMU
.................................................................
Chuo cha Misitu Olmotonyi kilichopo mkoani Arusha kimetakiwa kuboresha taaluma na mitaala ya kufundishia iweze kukidhi mahitaji ya jamii ya sasa na ijayo ikiwemo kujibu kero na changamoto zinazoikabili jamii hiyo.



Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipotembelea chuo hicho jana kwa ajili kukagua maendeleo yake na kuzungumza na waalimu pamoja na wafanyakazi ambapo pia alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa chuoni hapo ikiwemo ya bweni na ukumbi wa mihadhara.



Alisema Tanzania ya leo inahitaji wataalamu watakaojibu kero na kutatua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya uhifadhi nchini ikiwemo ya uharibifu wa misitu kwa njia ya uchomaji wa mkaa, uvunaji haramu wa magogo na vitendo vya uingizaji wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimpa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel (kushoto) ambayo inajenga mradi wa bweni na ukumbi wa mihadhara katika Chuo cha Misitu Olmotonyi alipotembelea chuo hicho jana mkoani Arusha. Aliitaka kampuni hiyo iharakishe kumaliza ujenzi wa mradi huo.

"Ni lazima muwafundishe wanafunzi wenu uaminifu na uzalendo wa kutumia rasilimali za misitu kwa njia endelevu, muwafundishe uhifadhi zaidi na sio uvunaji pamoja kutumia sheria ipasavyo katika kulinda na kusimamia rasilimali hizi huku wakitambua kuwa rasilimali hizo zikitoweka hakuna maisha kutokana na umuhimu wake katika maisha ya binadamu" alisema Prof. Maghembe.

Pamoja na hayo, alikitaka chuo hicho kujiimarisha zaidi katika mafunzo kwa vitendo kufikia viwango bora vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza waalimu kitaaluma kwa kutumia fursa mbalimbali ikiwemo za mafunzo ya nje ya nchi kwa mfumo wa "Scholarships". 

Aidha, alikitaka pia chuo hicho kujikita zaidi katika utoaji wa huduma kwa jamii katika sekta ya misitu pamoja na kuanzisha na kuimarisha programu mbalimbali za utafiti ambazo pamoja na faida nyingine pia zitakitangaza chuo hicho ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na waalimu na wafanyakazi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi mkoani Arusha jana . Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Christognus Haule.

Katika hatua nyingine, Prof. Maghembe amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya United Builders Ltd, Harshad Patel kukamilisha haraka ujenzi unaoendelea wa jengo la bweni na ukumbi wa mihadhara chuoni hapo. Ujenzi huo upo chini ya mradi wa ECOPRC na jengo la bweni litakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 100 na ukumbi wa mihadhara wanafunzi 200. 

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI


Hivyo makala CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE

yaani makala yote CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/chuo-cha-misitu-olmotonyi-chatakiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CHUO CHA MISITU OLMOTONYI CHATAKIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA - PROF. MAGHEMBE"

Post a Comment